Ama kwa hakika maradhi humfanya mtu kubaki kama mtumwa na ambaye hana lake humu duniani. Ugonjwa waeza kumfanya mtu awe kama asiyejiweza na wakati huo kuwapea watu wengi mzigo maishani. Watu wengi husema badala ya kuwa mgonjwa na kuwa mzigo kwa jamaa zako bora kufariki mara moja ili kuwaepushia mzigo. Hii ndio ilikuwa kauli ya mama yangu mzazi amabpo mara tu alipooza miguu yake ikafura asiweze hata kutembea kwa vyovyote vile. Miguu yake ilikuwa imefura ajabu jambo lililopelekea yeye kuiacha kazi yake aliyokuwa ameajiriwa katika afisi moja ya serikali mjini Kitale. Alikuwa mjane ambapo baba yetu alikuwa keshafariki kutokana na ajali na tulimtegemea mama kama aliyekimu mahitaji ya familia yetu. Siku ziliposonga miguu yake ile ilianza kunyauka na kutoka ngozi ya juu alibaki kulalamikia machungu kila mara kwani hata kuvaa viatu ilikuwa ni kibarua kigumu. Miguu ili jinsi siku zilivyopita ndipo zilikuwa hata nzito zaidi.